has gloss | swa: "World of Our Own" ni wimbo kutoka kwa kundi la Westlife, wimbo huu pia ndio umebeba jina la albamu yao ya "World of Our Own". Wimbo huu ulitoka kama single mwaka 2002. Wimbo huu ulitumika katika kituo cha televisheni cha Disney Channel Original Movie katika filamu ya You Wish!. "World of Our Own" ulishika nafasi ya #1 nchini Uingereza na kuwa wimbo wa 10 kutoka katika kundi hili kufikai katika nafasi ya kwanza. Wimbo huu ulishika nafasi ya 40 katika single zilizoongoza kwa mauzo kwa mwaka 2002 nchini Uingereza, kwa kufanikiwa kuuza zaidi ya nakala 200,000 |